ili Tor ifanye kazi kwa kila mtu, inahitaji kuzungumza lugha za kila mtu. Timu yetu ya utafsiri ya kujitolea inafanya kazi kwa bidii ili kufanya hili liwe kweli, na tunaweza kutumia usaidizi zaidi kila wakati. Vipaumbele vyetu vya sasa vya tafsiri ni kutafsiri Tor Browser, hati za Kivinjari cha Tor, na tovuti ya Mradi wa Tor, lakini kuna hati zingine nyingi ambazo tunaweza kutumia kusaidia kutafsiri pia.
Jifunze jinsi ya kujiandikisha na kuanza kuchangia.
Sijui pakuanzia? Hapa unaweza kupata muhtasari wa hali ya sasa ya localization kwa miradi tofauti ya Tor Project.
Kila ijumaa ya wiki ya 3 ya mwezi timu ya Tor L10n hukutana na kutafsiri pamoja, kubadilisha mbinu, kufurahi huku wakitafsiri, kukutana na watafsiri wenzako, na kufahamu vipaumbele vya l10n katika Tor Project.
Wakati mwingine tafsiri za programu tumizi hazifanyi kazi ipasavyo, Hapa unaweza kujifunza kuzirekebisha.
Ujanibishaji ni mchakato endelevu katika programu zetu zote. Je umeona maboresho yoyote tunayoweza kufanya kwa tafsiri zetu? Fungua tikiti, wasiliane nasi au uwe sehemu ya kikosi chetu cha watafsiri.