1. Wezesha usasishaji wa kiotomatiki wa programu
Mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuweka rilei yako salama ni kusakinisha masasisho ya usalama kwa wakati unaofaa na kiotomatiki ili usiweze kusahau kuihusu.
Fuata maagizo ya kuwezesha kusasisha programu ya kiotomatiki ya mfumo wa uendeshaji.
2. Sakinisha tor
Ili kusakinisha kifurushi cha tor
kwenye Arch Linux, tafadhali endesha:
# pacman -Syu tor
3. Sanidi /etc/tor/torrc
Weka faili yako ya usanidi /etc/tor/torrc
katika mahali pake
Nickname myNiceRelay # Badilisha "myNiceRelay" iwe kitu unachopenda
ContactInfo your@e-mail #Andika barua pepe yako na ufahamu kuwa itachapishwa
ORPort 443 # Unaweza tumia bandari tofauti utakopotaka
ExitRelay 0
SocksPort 0
Log notice syslog
DataDirectory /var/lib/tor
User tor
4. Wezesha na uanzishe tor
# systemctl enable --now tor
... or restart it if it was running already, so configurations take effect
# systemctl restart tor
5. Maelezo ya mwisho
Ikiwa una shida kusanidi kiungo chako angalia sehemu yetu ya usaidizi.
Ikiwa kiungo chako kinajiendesha sasa tazama maelezo ya baada ya usakini.