1. Wezesha usasishaji wa kiotomatiki wa programu
Mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuweka rilei yako salama ni kusakinisha masasisho ya usalama kwa wakati unaofaa na kiotomatiki ili usiweze kusahau kuihusu.
Fuata maagizo ya kuwezesha kusasisha programu ya kiotomatiki ya mfumo wa uendeshaji.
2. Sakinisha tor
Kusakinisha kifurushi cha tor
kwa Void Linux, tafadhali endesha:
# xbps-install -S tor
3. Sanidi /etc/tor/torrc
Weka faili yako ya usanidi /etc/tor/torrc
katika mahali pake
Nickname myNiceRelay # Badilisha "myNiceRelay" iwe kitu unachopenda
ContactInfo your@e-mail #Andika barua pepe yako na ufahamu kuwa itachapishwa
ORPort 443 # Unaweza tumia bandari tofauti utakopotaka
ExitRelay 0
SocksPort 0
Log notice syslog
DataDirectory /var/lib/tor
User tor
4. Wezesha na uanzishe tor
Tofauti na usambazaji wa hivi majuzi Void Linux haitumii systemd; inatumia runit badala yake.
Kuwezesha huduma ya tor
kwenye mfumo uliowashwa:
# ln -s /etc/sv/tor /var/service/.
Mara tu baada ya kuwezesha huduma itaanza moja kwa moja. Ikiwa tayari umeanzisha daemon ya tor
hapo awali na ulifanya mabadiliko kufanya usanidi wake unaweza kuianzisha tena kwa:
# sv restart tor
5. Maelezo ya mwisho
Ikiwa una shida kusanidi kiungo chako angalia sehemu yetu ya usaidizi.
Ikiwa kiungo chako kinajiendesha sasa tazama maelezo ya baada ya usakini.