Mwongozo huu utakusaidia kusanidi kiungo cha WebTunnel kwa kutumia Docker kusaidia watumiaji waliodhibitiwa kuunganishwa kwenye mtandao wa Tor.

0. Sanidi kikoa chako na seva ya tovuti yako

Kabla ya kuendelea na maagizo yaliyo hapa chini, ni muhimu kusanidi kikoa chako na seva ya wavuti kwanza. Rejelea sehemu ya kwanza ya mwongozo wa WebTunnel ili kuona jinsi ya kusanidi kikoa cha tovuti yako na seva ya wavuti.

1. Sakinisha wakati wa kuendesha Docker

Maelekezo katika hatua hii ni ya mifumo inayotumia Debian, lakini unaweza kupata maelekezo ya Docker kwa mifumo mingine inayotumika.

# apt install curl sudo
$ curl -fsSL https://get.docker.com -o get-docker.sh
$ sudo sh ./get-docker.sh

2. Endesha kiungocha Dockerized WebTunnel

Badilisha URL na kikoa chako na njia (rejelea sehemu ya kwanza ya mwongozo wa WebTunnel), na OPERATOR_EMAIL na anwani yako ya barua pepe, kisha endesha:

$ truncate --size 0 .env
$ echo "URL=https://yourdomain/and/path" >> .env
$ echo "OPERATOR_EMAIL=your@email.org" >> .env
$ echo "BRIDGE_NICKNAME=WTBr$(cat /dev/urandom | tr -cd 'qwertyuiopasdfghjklzxcvbnmMNBVCXZLKJHGFDSAQWERTUIOP0987654321'|head -c 10)" >> .env
$ echo "GENEDORPORT=4$(cat /dev/urandom | tr -cd '0987654321'|head -c 4)" >> .env

Amri hizi zitaunda faili ya mazingira (.env) kwa ajili ya usanidi wa kiungo cha WebTunnel.

3. Pakua faili ya utunzi ya WebTunnel docker

$ curl https://gitlab.torproject.org/tpo/anti-censorship/pluggable-transports/webtunnel/-/raw/main/release/container/docker-compose.yml?inline=false > docker-compose.yml

4. Anzisha kiungo chako cha WebTunnel

docker compose up -d

Kumbuka kuwa faili hii ya utunzi wa Docker inajumuisha kusasisha kiotomatiki kwa chaguo-msingi, na itasasisha seva ya kiungo cha WebTunnel bila hatua yoyote zaidi. Toa watchtower kudhibiti tabia hii.

5. Hariri kiungo chako cha WebTunnel

Unaweza kupata anwani yako ya kiungo na uthibitishe ikiwa inafanya kazi kwa kuendesha:

$ docker compose exec webtunnel-bridge get-bridge-line.sh

Unaweza kunakili na kubandika mstari wa kiungo kwenye Kivinjari cha Tor (Alpha), na inapaswa kufanya kazi. Kwa chaguomsingi, kiungo chako cha kituo cha WebTunnel litasambazwa kupitia tovuti ya Viungo.